Saturday, February 4, 2012

Nani anafaa kuongezewa posho katika hawa wafuatao!


Wako bungeni,halafu ona madarasa ya watoto wetu!
Miaka hamsini tunakaa chini,watoto wetu hawana madawati,
Hiyo ndio shule bwana,daktari wa maana atatoka wapi?
Na hilo darasa umelionaje?
Wakifaulu katika shule za kata madarasa ndio hayo!
Na wakina mama ambao ndio inasemekana ndio wapigajia kura wengi wa chama tawala hospitalini wwanahudumiwa hivi
Ndio,hapa tunstahili sisi na mama zetu na dada zetu,wao wakiumwa mafua wanapelekwa INDIA.
Vitanda pia vimetushinda,VX  V8 wameweza kununua.
Balaa tupu,kama mafungu ya nyanya,kumbe hospitali.
Maji ndio kabisa
Umemuona kada huyo akinywa maji?
Cheki walivyonenepa,hawana njaa asilani,
Wanajifanya wako pamoja na sisi,
Wameshiba mpaka wanalala
Na huu ni msimu wa wao kuvuna na kutudanganya!
Wakati wanaambiana wanafikiria kwa kutumia masaburi,kazi ipo!
Kalala fofofo,unafikiri atakumbuka hata yanayoongelewa hapo bungeni?angekuwa na njaa wala asingelala.....